Mapambano kati ya Israeli na Palestina

Mapambano kati ya Israeli na Palestina ni ugomvi baina ya nchi ya Israeli na wakazi wa Palestina unaoathiri pia uhusiano na nchi jirani. Ugomvi huu ulianza katika karne ya 20 baina ya wakazi Wayahudi na Waarabu wa maeneo ambayo leo hii yako chini ya Israeli na Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina. Ulisababisha tayari vita sita kati ya nchi ya Israeli tangu kuundwa kwake mwaka 1948 na jirani zake za Kiarabu. Mapambano yanaendelea, hayajapata suluhisho hadi sasa. Mapambano yalianza wakati wa kuongezeka kwa uhamiaji wa Wayahudi katika maeneo ya Palestina yaliyokaliwa na Waarabu. Kuundwa kwa Dola la Israeli kulisababisha vita ya kwanza baina ya Israeli mypa na nchi zote za jirani. Hivyo ilikuwa pia chanzo cha mgongano kati ya Israeli na nchi za Waarabu kwa jumla.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search